Hohenzollernbruecke Bridge - The Bridge of Love
| | ||
| |
Jiamini unaweza na ufanye unachoamini!!
KAMATI ya Bunge ya Hesabu za Mashirika ya Umma(PAC), imeagiza kwamba sheria inayoruhusu Mamlaka ya Nishati na Madini(EWURA) kulipa mishahara ya watumishi wa Baraza Ushauri na Watumaji la Nishati na Madini (EWURA CCC) ibadilishwe ili baraza hilo liweze kufanya kazi ipasavyo.
Hayo yalisemwa leo na Makamu Mwenyekiti wa PAC, Deo Filikunjombe wakati akizungumza na waandishi wa habari leo kwenye ofisi ndogo za Bunge jijini Dares Salaam kuhusu shughuli zilizofanywa na kamati yake , ambapo alisema baraza hilo hesabu zake zinakwenda vizuri.
“Baraza hili hesabu zake ni nzuri , lakini halifanyi kazi ipasavyo kwa kuwa halimtendei kazi ipasavyo liko pamoja na EWURA tumeagiza sheria ibadilishwe ili liweze kufanya kazi kwa kuzingatia pande zote,” alisema Filikunjombe.
Makamu Mwenyekiti huyo alishauri kuwa ni vyema mishahara hiyo ilipwe na wizara husika ili baraza hilo lifanye kazi bila kuegemea upande mmoja.
Akizungumzia kuhusu upandaji wa umeme kwa asilimia 40 alihojia upanda kwa sababu zipi je mlaji wa chini wamemsikiliza wanasemaje, hivyo alisema haitakuwa sahihi ikiwa hakusikilizwa.
Aliongeza kuwa baraza hilo pia linatakiwa kuacha kulipa malipo ya kila baada ya miaka mitano mtumishi anapostaafu badala yake yawe katika mfumo ya mifuko ya hifadhi ya jamii, ikiwemo kuwaingiza watumishi wake katika Mfuko wa Bima ya Afya ili kuepuka utumiaji wa risiti za malipo ya matibabu.
Alitaka baraza hilo kutumia fedha kulingana na bajeti yake.
Wakati huohuo Filikunjombe alisema kamati hiyo imemfukuza mwakilishi wa Shirika Hodhi la Mali za Umma (CHC) kwa kuwa ni mtendaji wa chini hawawezi kuzungumza naye hivyo wanamtaka Ofisa Mtendaji Mkuu.
Makamu Wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akikata utepe kuzindua rasmi Jengo la Ofisi ya Idara ya Maji, lililopo Wilaya ya Pangani, wakati alipoanza ziara yake ya Mkoa wa Tanga leo, Januari 24, 2012. Kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Chiku Galawa (kushoto) ni Mkurugenzi wa Maji wa wilaya hiyo, Mohamed Hamis. Picha na Muhidin Sufiani-OMR
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisikiliza maelezo kuhusu ukuta huo unaozuia maji ya Bahari unaobomoka kutokana na mabadiliko ya Tabia nchi na kutishia amani ya wakazi wa maeneo hayo. Pangani Kivukoni. Picha na Muhidin Sufiani-OMR
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiongozana na baadhi ya Viongozi wa Wilaya ya Pangani wakati akitoka kukagua ukuta wa kuzuia maji ya Bahari unaobomoka Pangani Kivukoni. Picha na Muhidin Sufiani-OMR
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiangalia ukuta unaozuia maji ya Bahari eneo la Pangani Kivukoni, unaozidi kubomoka kutokana na kujengwa miaka 100 iliyopita na kutishia amani kwa wakazi wa maeneo hayo. Makamu wa Rais ameanza ziara yake ya Mkoa wa Tanga leo Januari 24, 2012. Picha na Muhidin Sufiani-OMR 
Siku chache baada ya Chama cha Madaktari nchini (MAT) kutangaza mgogoro na serikali na kuipa saa 72, serikali imetangaza kuwa ipo tayari kukaa nao meza moja na kuzungumzia masuala ya sekta ya afya.
Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Lucy Nkya, alitoa kauli hiyo jana na kusema kuwa serikali ipo tayari kukaa na MAT kuzungumza kama watakuwa tayari.
Dk. Nkya alisema sakata la madaktari 1,994 waliokuwa katika mazoezi katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili waliamua kutoendelea na ratiba zao za mazoezi kwa vitendo baada ya kucheleweshewa posho zao za kila mwezi.
Alisema baada ya kuchelewa kutolewa kwa fedha za posho, wizara ilifanya jitihada ya kuhakikisha fedha hizo zinapatikana haraka.
Alisema serikali ilikuwa ikitoa taarifa katika taasisi walizokuwa wakifanyia kazi kuhusiana na jitihada zinazofanywa ili kutatua tatizo hilo.
“Ieleweke kwamba wataalamu hawa huingia mikataba na hospitali husika na mkataba wanaoingia umeainisha hawatakiwi kugoma au kuanzisha mgomo,” alisema Dk. Nkya.
Dk. Nkya alisema pamoja na wizara kufanya jitihada hizo kuwa suala lao limefanyiwa ufumbuzi, lakini bado walishikilia msimamo wao wa kutorudi vituoni hadi wapokee fedha na kwamba jambo hilo halikuwa la kiungwana.
Alisema baada ya kuona hivyo, wizara ilipeleka wataalamu 51 waliokuwa wakisubiri kuanza mafunzo Januari mwaka huu ili kuchukua nafasi za wataalamu waliokataa kurejea katika hospitali hiyo kwa ajili ya kuzuia athari ambazo zingeweza kujitokeza kwa wagonjwa. Hata hivyo, alisema katika mgomo huo kuna wenzao 60 ambao hawakugoma.
“Baadhi ya wataalamu waliokuwa wakifanya mazoezi katika vituo kama vya Hospitali ya KCMC, Mount Meru, Bombo, Bugando na Manispaa za Dar es Salaam walitambua jitihada za wizara za kushughulikia tatizo hilo na waliendelea na ratiba yao ya mazoezi kwa vitendo,” alisema.
Alisema waliogoma uongozi wa Muhimbili uliwachukulia hatua na kuwaandikia barua kuwarudisha wizarani na kutaka wapatiwe wataalamu hao.
“Ili kuhakikisha wataalamu hao wanafikia malengo ya mazoezi ya vitendo wizara imeamua kuwapanga katika hospitali mbalimbali ikiwemo Muhimbili, Temeke, Mwananyamala, Aga khan, Amana na Lugalo kwa kuzingatia uwezo wa hospitali,” alisema.
Alisema Januari 16, mwaka huu wataalamu 194 walikuwa wamepewa barua na wameripoti katika vituo walivyopangiwa.
Alisa wizara yake imepata taarifa kupitia vyombo vya habari kuwa MAT imewapa saa 72 iwarudishe madakatari hao katika hospitali ya Muhimbili pamoja na kutaka kuondolewa kwa baadhi ya viongozi wa wizara.
Hata hivyo, alisema tamko hilo halijawasilishwa rasmi wizarani na kusisitiza kuwa madakatari hao hawajafukuzwa kufanya mazoezi bali wamepangiwa vituo vingine.
Akizungumzia uamuzi wa MAT kumvua uanachama Mganga Mkuu wa Serikali, Deo Mtasiwa, Dk. Nkya alisema chama hicho hakiwezi kumchukulia hatua bali chombo chenye mamlaka ni Wizara.
Rais wa MAT, Dk. Namala Mkopi, alisema suala hilo watalizungumzia leo na kwamba tamko walilolitoa Jumamosi sio lazime lipelekwe wizarani ndio maana walitoa taarifa kupitia vyombo vya habari.